Jumatano, 27 Aprili 2016

Habari zetu Tanzania media Tv leo-TUGHE WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAKUTANA KUCHAGUA MFANYAKAZI BORA WA TAWI LA WIZARA HIYO.

Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi (kulia meza kuu) akizungumza na wajumbe wa chama hicho kabla ya kufanya uchaguzi wa Mfanyakazi Bora wa tawi hilo katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto meza kuu ni Katibu wa Chama hicho, Obed Mbaga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), tawi la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, William Mkombozi (kulia meza kuu) akizungumza na wajumbe wa chama hicho kabla ya kufanya uchaguzi wa Mfanyakazi Bora wa tawi hilo katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto meza kuu ni Katibu wa Chama hicho, Obed Mbaga. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


Habari zetu Tanzania media Tv leo-WANAMTANDAO WAITAKA DAWASCO KUTUPIA JICHO TABAKA LA WASIOJIWEZA

Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maji safi na Usafi wa Mazingira jijini Dar es Salaam (DAWASCO) Mhandisi Cyprian Luhemeja akifurahia jambo na ujumbe kutoka  Mtandao Kijinsia Tanzania (TGNP) walipofika ofsini hapo kwa ajili ya kutoa shukrani zao.
Mwanaharakati kutoka mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP), Bi Gema Akilimali akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa shukrani
fupi kwa uongozi wa DAWASCO kutokana na jitihada zilizofanyika katika kuboresha huduma ya Majisafi na Majitaka Jijini Dar es salaam hususani maeneo ya wananchi wenye kipato cha chini. Kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco Mhandisi Cyprian Luhemeja.
 

WANAHARAKATI WA Mtandao wa kijinsia “TGNP” wamepongeza juhudi zinazofanywa na Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (Dawasco), kutokana na Mabadiliko na jitihada zinazofanywa na Dawasco za kuboresha huduma ya Maji pamoja na kufanya kazi za kusaidia jamii inayoizunguka.

Akizungumza katika kikao cha pamoja na Dawasco, Mratibu wa kampeni ya Maji ya “MAMA TUA NDOO KICHWANI” kutoka Mtandao wa Kijinsia Bi. Martha Samwel.

Ameitaka Dawasco kuhakikisha inapeleka huduma ya Majisafi na salama katika sehemu zote muhimu ikiwamo mashuleni na hospitalini ili kumpunguzia mwanamke adha ya kutafuta Maji kutoka umbali mrefu pamoja na kumuondolea mwanamke adha ya kubakwa na hata kupigwa kutokana na kuhangaika kutafuta Maji.

“Tunataka kutoa salamu za pongezi kwa DAWASCO kwa mabadiliko na jitihada tunazoziona za kuboresha huduma ya Maji na kufanya kazi ya kusaidia jamii, tumefurahishwa na jitihada zenu,tutafanya kazi pamoja ili kuhakikisha tunamuondolea mwanamke shida ya kupoteza muda mwingi kuhangaika kutafuta Maji kwani kampeni yenu ya “ MAMA TUA NDOO YA MAJIKICHWANI” ndio kampeni yetu” alisema Bi. Martha.

Aidha, Mwanaharakati wa mtandao wa kijinsia Bi. Gema Akilimali, amefurahishwa ya kampeni ya Mama tua ndoo kichwani kwani itamsaidia mwanamke kwa kiasi kikubwa kushiriki kikamilifu katika kujenga uchumi wa nchi, kitendo ambacho kwa sasa hatimizi ipasavyo kutokana na kutumia muda mwingi kutafuta maji, pia anaamini utaongeza ufaulu mashuleni kwani badala ya watoto wa kike kutumia muda mwingi kutafuta Maji sasa wataweza kuokoa muda na kuwa kushiriki masomo ipasavyo.

Habari zetu Tanzania media Tv leo-MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA UONGOZI WA BARAZA LA TAWLA NA UONGOZI WA SKAUT LEO

mak1 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na uongozi wa Baraza la Wanachama wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) wakati Uongozi huo ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 27,2016 kwa lengo la kumpongeza na pamoja na kumuelezea malengo na mikakati ya kiutendaji ya Chama hicho.
mak2
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Baadhi ya Wawakilishi na Wanachama wa Chama cha SKAUT Nchini wakati ujumbe wa wawakilishi hao ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es salaam leo April 27,2016 kwa ajili ya kumuelezea Makamu wa Rais shuhuli zao za kiutendaji hasa katika kutoa mafunzo mbalimbali kwa Mtoto wa kike.
mak3
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa SKAUT Nchini.Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Wanachama wa SKAUT Nchini.
mak4
Makamu wa Rais Mhe. Samia akiwa katika picha ya pamoja na Uongozi wa Baraza la TAWLA
mak6
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiungumza na Katibu Mkuu Kiongozi Baolozi Peter Kijazi Baada ya kuapishwa kwa Makatibu wa Mikoa leo April 27,2016 Ikulu Dar es salaam. (Picha na OMR)

Habai zetu leo, Tanzania Media Tv-SERIKALI YAZUIA UINGIZAJI HOLELA WA MCHELE

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameviagiza vyombo vya dola viimarishe ulinzi kwenye mipaka ya nchi na hasa katika mwambao wa Bahari ya Hindi ili kuzuia uingizwaji holela wa mchele wa magendo kutoka nje ya nchi.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumatano, Aprili 27, 2016) wakati akijibu hoja za wabunge na kuhitimisha hoja ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2016/2017 bungeni mjini Dodoma.

“Napenda kuviagiza vyombo vya dola viendelee kuimarisha ulinzi wa mipaka yetu hasa katika mwambao wa Bahari ya Hindi ili kuzuia uingizwaji holela wa mchele wa magendo kutoka nje ya nchi. Endapo patatokea upungufu wa mchele nchini, Serikali itaangalia uwezekano wa kuruhusu kuagiza mchele kutoka nje,” amesema.

Waziri Mkuu amesema katika kipindi cha miaka sita iliyopita, kumekuwa na ongezeko la asilimia 14 katika uzalishaji wa mpunga hapa nchini na hivyo kufanya kiwango cha uzalishaji kiwe ni kikubwa kuliko mahitaji.

“Takwimu za uzalishaji mpunga zinaonesha kuwepo ongezeko katika kipindi cha miaka sita iliyopita ambacho kiliongezeka kutoka tani 1,699,825 mwaka 2009/2010 hadi kufikia tani 1,936,909 mwaka 2014/2015 sawa na ongezeko la asilimia 14. Katika kipindi chote hicho, kiwango cha uzalishaji wa mpunga kimekuwa kikubwa kuliko mahitaji,” amesema.

“Kutokana na mwenendo huo mzuri wa uzalishaji wa mpunga hapa nchini, Serikali ilisitisha kutoa vibali vya kuagiza mchele kutoka nje ya nchi tangu Machi, 2013. Hatua hii itasaidia wakulima wetu kupata soko la uhakika na bei nzuri, jambo ambalo linawaongezea kipato na pia kuwahamasisha kuongeza uzalishaji zaidi,” amesema.

Akizungumzia kuhusu deni la sh. bilioni 134 ambalo Serikali inadaiwa na Bohari ya Dawa nchini (MSD), Waziri Mkuu alisema Serikali imeanza kulishughulikia deni hilo kwa kumwelekeza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ahakiki deni hilo. “Mpaka sasa CAG amehakiki madai ya jumla ya shilingi bilioni 67 na kazi ya uhakiki inaendelea.”

Akifafanua kuhusu vigezo vilivyutumika kugawanya majimbo mapya ya uchaguzi, Waziri Mkuu alisema mwaka 2015, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilipokea maombi 77 ya kuanzishwa majimbo mapya, ambapo Halmashauri 37 ziliwasilisha maombi ya kugawa majimbo ya uchaguzi na maombi 40 yalitoka katika majimbo yaliyokuwepo yakiomba kugawanywa. Kati ya maombi yaliyowasilishwa, maombi 35 tu ndiyo yalikidhi vigezo na yalistahili kugawanywa.

“Kutokana na ongezeko la Halmashauri mpya ambazo kisheria ni majimbo ya uchaguzi, ongezeko la idadi ya wabunge wanawake wa viti maalum na uwezo wa ukumbi wa Bunge; Tume iliamua kutumia vigezo vitatu tu ili kupata idadi ya majimbo yanayoweza kugawanywa. Vigezo hivyo ni: Wastani wa idadi ya watu (Population Quota), mipaka ya kiutawala na uwezo wa ukumbi wa Bunge,” alisema.

Waziri Mkuu alisema chini ya mchakato huo, Tume ilianzisha majimbo mapya 25 ambapo majimbo 19 yalitokana na ongezeko la Halmashauri mpya; na majimbo sita yalitokana na kigezo cha wastani wa idadi ya watu.

Hata hivyo, Waziri Mkuu alibainisha kwamba kwa sasa Serikali haina mpango wa kuongeza maeneo mapya ya utawala zikiwemo wilaya na mikoa mipya kwa sababu bado inaendelea kujengea uwezo wa rasilmali watu na vitendea kazi katika maeneo mapya ya utawala yaliyopo hivi sasa

Jumatano, 9 Machi 2016

WANAWAKE WOTE NCHINI WAMETAKIWA

 KWA hISANI YA RTV

Kuelekea siku ya wananawake duniani ambayo kila mwaka inafanyika Marchi 8, Wanawake wote nchini wametakiwa kujiamini na kuwa na uthubutu kwa kufanya shughuli za kujitafutia kipato kuliko kuwa tegemezi, katika kukabiliana na changamoto zinazowakabili  mbele yao katika maisha yao ya kila siku.
Rai hiyo ilitolewa na Mwanaharakati wa masuala ya wanawake na mfanyabiashara maarufu, anayeuza mafuta ya kuendeshea mitambo mbalimbali mkoani Ruvuma, Farida Mdaula wakati alipokuwa akizungumza na baadhi ya wanawake wa Manispaa ya Songea.